Jaku aiomba SMZ kuwekeza Ligi Kuu Zanzibar

Jun 10, 2026 - 18:15
0 0
Jaku aiomba SMZ kuwekeza Ligi Kuu Zanzibar

By  Zuleikha Fatawi

Reporter

Mwananchi Communications Limited

Mwakilishi wa Paje, Jaku Hashim Ayub ameishauri serikali kuwekeza fedha katika Ligi Kuu Zanzibar kwa lengo la kuipa thamani na ushindani kama zilivyo ligi nyingine.

Jaku alisema Ligi hiyo itafanyiwa uwekezaji mkubwa haitakuwa kama inavyoonekana kwasasa kwa kutokuwa na hamasa kwa wananchi kisiwani hapa.

Alisema, kitu chochote ili kifanikiwe lazima kipewe kipaumbele na uwekezaji mzuri utakaowavutia wadau kuwekeza.

“Ikiwa tumedhamiria kuwainua vijana wetu kiuchumi lazima Serikali iwekeze fedha kwa ajili ya ZPL kwani Ligi hiyo imetoa ajira kwa vijana wetu,” alisema

Mwakilishi huyo, alisema Ligi Kuu ya Zanzibar kwa sababu ya kutokuwa na uwekezaji mzuri na ndio maana watu hawaifutalii.

Mbali na hilo, Jaku aliiomba Serikali kuirejesha ligi ya vijana kwani ndio inayozalisha wachezaji wengi wenye uwezo na wanaoiwakilisha Zanzibar kitaifa na kimataifa.

Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0