{"id":831,"date":"2026-08-27T09:21:56","date_gmt":"2026-08-27T09:21:56","guid":{"rendered":"https:\/\/spotileo.co.tz\/?p=22778"},"modified":"2026-08-27T09:21:56","modified_gmt":"2026-08-27T09:21:56","slug":"simba-coastal-kazi-ipo-leo","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/simba-coastal-kazi-ipo-leo\/","title":{"rendered":"Simba, Coastal kazi ipo leo"},"content":{"rendered":"\n<p><strong>DAR ES SALAAM:<\/strong> SIMBA leo itakuwa na kazi ya kuendeleza mwanzo wake mzuri wa Ligi Kuu msimu wa 2026\/27, itakapokutana na Coastal Union katika mchezo wa raundi ya nne utakaopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kuanzia saa 1:00 usiku.<\/p>\n<p>Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza, huku ikifunga mabao matano na kuruhusu moja pekee. Ushindi wa leo utaifanya ifikishe pointi 12 na kuendelea kuibana Yanga kileleni.<\/p>\n<p>Kocha wa Simba, Steven Barker, amesisitiza umuhimu wa timu yake kuendelea kukusanya pointi nyingi katika mwanzo huu wa msimu ili kujenga msingi mzuri wa kuwania ubingwa.<\/p>\n<p>\u201cLengo letu ni kupata pointi nyingi katika michezo hii. Tunataka kushinda michezo yetu na hilo litatupa nafasi nzuri. Huu ni mwanzo mzuri kwetu na tunapaswa kuendelea kujenga kutoka hapa,\u201d alisema Barker.<\/p>\n<p>Hata hivyo, changamoto kubwa kwa Simba katika mchezo huo inaweza kuwa nidhamu, baada ya kuanza msimu kwa kasi isiyotarajiwa upande wa kadi nyekundu.<\/p>\n<p>Katika mechi tatu za mwanzo, Simba imepoteza wachezaji watatu kwa kadi nyekundu, ambapo David \u2018Duchu\u2019 Kameta alioneshwa nyekundu dhidi ya Kagera Sugar, Ibraheem Jabaar dhidi ya Pamba Jiji na Anthony Mligo kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars.<\/p>\n<p>Hilo ni jambo ambalo Barker atalazimika kulidhibiti ili kikosi chake kiweze kuendelea kucheza kwa nguvu bila kujikuta kikicheza pungufu kwa idadi ya wachezaji.<\/p>\n<p>Kwa upande mwingine, Coastal Union inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na presha kubwa baada ya kuvuna pointi moja pekee katika mechi tatu, hali inayoiweka nafasi ya 14 kwenye msimamo.<\/p>\n<p>Coastal Union imefunga mabao mawili na kufungwa sita, hivyo leo itakuwa na jukumu la kuzuia Simba isiongeze matatizo yake huku ikitafuta ushindi wake wa kwanza msimu huu.<\/p>\n<p>Ingawa takwimu zinaipa Simba nafasi kubwa ya kushinda, Coastal Union inaweza kutumia presha iliyonayo kama motisha ya kufanya vizuri na kushtua wapinzani wao.<\/p>\n<p>Katika michezo mitano iliyopita kati ya timu hizo, Simba imeshinda minne huku mchezo mmoja ukiisha kwa sare, rekodi inayoongeza matumaini kwa mashabiki wake kabla ya mpambano huo.<\/p>\n<p>Kabla ya mchezo huo, Mashujaa itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Lake Tanganyika kuanzia saa 10:00 jioni.<\/p>\n<p>Mashujaa iko nafasi ya tisa ikiwa na pointi tatu, wakati Kagera Sugar iko nafasi ya 15 ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tatu.<\/p>\n<p>Mwisho<\/p>\n<p>The post <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\/simba-coastal-kazi-ipo-leo\/\">Simba, Coastal kazi ipo leo<\/a> first appeared on <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\">SpotiLEO<\/a>.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"\n<p><a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\/simba-coastal-kazi-ipo-leo\/\"><\/p>\n<p><strong>DAR ES SALAAM:<\/strong> SIMBA leo itakuwa na kazi &#8230; <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\/simba-coastal-kazi-ipo-leo\/\" class=\"read-more\">Read the rest <\/a><\/p>\n<p><\/a><\/p>\n<p>The post <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\/simba-coastal-kazi-ipo-leo\/\">Simba, Coastal kazi ipo leo<\/a> first appeared on <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\">SpotiLEO<\/a>.<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_monsterinsights_skip_tracking":false,"footnotes":""},"categories":[19],"tags":[],"class_list":["post-831","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-spoti"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/831","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=831"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/831\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=831"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=831"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=831"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}