{"id":939,"date":"2026-09-03T08:48:37","date_gmt":"2026-09-03T08:48:37","guid":{"rendered":"https:\/\/spotileo.co.tz\/?p=22954"},"modified":"2026-09-03T08:48:37","modified_gmt":"2026-09-03T08:48:37","slug":"chidy-benz-wasanii-tulinde-maadili-kwa-vizazi-vyetu","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/chidy-benz-wasanii-tulinde-maadili-kwa-vizazi-vyetu\/","title":{"rendered":"Chidy Benz: Wasanii tulinde maadili kwa vizazi vyetu"},"content":{"rendered":"\n<p><strong>DAR ES SALAAM:<\/strong> Msanii wa Bongo Fleva nchini, Rashid Chidy Benz, amewataka wasanii wenzake kuzingatia na kulinda maadili katika jamii, akisisitiza kuwa wasanii nao ni wazazi na wana wajibu wa kuhakikisha wanajenga mazingira bora kwa vizazi vya sasa na vijavyo.<\/p>\n<p>Chidy Benz ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuitikia wito wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Propas Katambi, aliyewaita wasanii kwa ajili ya semina kuhusu maadili na uelewa wa Katiba.<\/p>\n<p>Amesema wasanii ni kioo cha jamii, hivyo wanapaswa kuwa makini na mambo wanayoyaonesha na kuyashiriki, hususan kupitia mitandao ya kijamii, kwa kuwa yanaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa jamii.<\/p>\n<p>\u201cSisi wasanii ni wazazi pia, tuna watoto. Kwa hiyo tunatakiwa kulinda maadili kwa ajili ya vizazi vyetu vya sasa na vya baadaye.<\/p>\n<p>Kama wasanii ni kioo cha jamii, tunapaswa kuzingatia maadili, hasa katika mitandao yetu ya kijamii,\u201d amesema Chidy Benz.<\/p>\n<p>Aidha, Chidy Benz amesema yuko tayari kuwa balozi wa maadili miongoni mwa wasanii, akiahidi kuhamasisha wasanii wenzake kuhakikisha wanazingatia maadili katika kazi zao na matumizi ya mitandao ya kijamii.<\/p>\n<p>Amesema semina hiyo imewapa wasanii uelewa muhimu kuhusu wajibu wao katika jamii na umuhimu wa kusimamia maadili, akisisitiza kuwa ujumbe huo tayari umefika na sasa ni wakati wa kuufanyia kazi.<\/p>\n<p>\u201cNitakuwa balozi wa maadili na nitawahamasisha wasanii wenzangu kusimamia maadili, kwa sababu tumeshapata ujumbe na tumeambiwa tayari. Sasa ni wajibu wetu kuutekeleza,\u201d amesema.<\/p>\n<p>The post <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\/chidy-benz-wasanii-tulinde-maadili-kwa-vizazi-vyetu\/\">Chidy Benz: Wasanii tulinde maadili kwa vizazi vyetu<\/a> first appeared on <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\">SpotiLEO<\/a>.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"\n<p><a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\/chidy-benz-wasanii-tulinde-maadili-kwa-vizazi-vyetu\/\"><\/p>\n<p><strong>DAR ES SALAAM:<\/strong> Msanii wa Bongo Fleva nchi&#8230; <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\/chidy-benz-wasanii-tulinde-maadili-kwa-vizazi-vyetu\/\" class=\"read-more\">Read the rest <\/a><\/p>\n<p><\/a><\/p>\n<p>The post <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\/chidy-benz-wasanii-tulinde-maadili-kwa-vizazi-vyetu\/\">Chidy Benz: Wasanii tulinde maadili kwa vizazi vyetu<\/a> first appeared on <a href=\"https:\/\/spotileo.co.tz\">SpotiLEO<\/a>.<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_monsterinsights_skip_tracking":false,"footnotes":""},"categories":[19],"tags":[],"class_list":["post-939","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-spoti"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/939","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=939"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/939\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=939"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=939"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/sokasoga.website\/ltv\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=939"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}