Marekani Yafungua Kombe la Dunia Nyumbani Kwa Kishindo, Yaichapa Paraguay 4-1

Jun 13, 2026 - 13:15
0 0
Marekani Yafungua Kombe la Dunia Nyumbani Kwa Kishindo, Yaichapa Paraguay 4-1

Global Publishers June 13, 2026 0 Comments

SHARE THIS:

Katika dimba la SoFi Stadium, timu ya taifa ya Marekani ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa ushindi mkubwa wa mabao 4-1 dhidi ya Paraguay usiku wa Ijumaa.

Nyota wa Marekani, Folarin Balogun, aliibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza, huku Marekani ikitengeneza historia kwa kuongoza kwa mabao 3-0 kabla ya mapumziko, ikiwa ni mara ya kwanza kufunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa Kombe la Dunia.

Nahodha Christian Pulisic alikuwa katika kiwango cha juu, akitoa pasi za mabao na kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Marekani iliyowapa furaha mashabiki zaidi ya 70,000 waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.

Bao la kwanza la Marekani lilitokana na kujifunga kwa kiungo wa Paraguay, Damiรกn Bobadilla, kabla ya Balogun kuongeza mawili dakika ya 31 na dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilishuhudia Paraguay ikipata bao la kufutia machozi kupitia Mauricio, lakini Gio Reyna aliihakikishia Marekani ushindi mnono kwa kufunga bao la nne katika dakika za mwisho za mchezo.

Ushindi huo ulikuwa wa kihistoria kwa Marekani kwani ni mara ya kwanza kufunga mabao manne katika mchezo mmoja wa Kombe la Dunia, huku pia ukiwa ushindi wake mkubwa zaidi katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo tangu yaliporejea kuandaliwa nyumbani kwao baada ya miaka 32.

Marekani chini ya kocha Mauricio Pochettino imeonyesha sura mpya ya ushambuliaji, jambo linalowapa matumaini makubwa mashabiki wao katika safari ya kusaka ubingwa wa dunia.

Mchezo huo pia ulihudhuriwa na watu maarufu mbalimbali kutoka Hollywood na sekta nyingine, akiwemo Tom Cruise, George Lucas, Bill Gates, Halle Berry, Leonardo DiCaprio na Kareem Abdul-Jabbar.

SHARE THIS:

Comments (0)

User
๐Ÿ”’
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI โ€” NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

โœ… HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
โœ… MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
โœ… KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
โœ… KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
โœ… KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0