Vita ya pointi tatu, Yanga kukabiliana na Mashujaa Kigoma
Muktasari:
- Katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini, Kigoma, Yanga inaingia iki-hitaji kuendeleza tena wimbi la ushindi na kujikita kileleni mwa msimamo, huku kwa upande wa Mashujaa ikipambana kulipiza kisasi cha mabao 6-0.
LIGI Kuu Bara inaendelea leo kwa mechi tatu kupigwa kwenye viwanja mbalimbali na mabingwa wate-tezi Yanga iliyo kileleni mwa msimamo na pointi 60 chini ya Kocha Abdihamid Moalin itakuwa na kibarua ugenini cha kupambana na Mashujaa FC ya Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ saa 10:15 jioni.
Katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini, Kigoma, Yanga inaingia iki-hitaji kuendeleza tena wimbi la ushindi na kujikita kileleni mwa msimamo, huku kwa upande wa Mashujaa ikipambana kulipiza kisasi cha mabao 6-0.
Mechi ya raundi ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Yanga ilishinda mabao 6-0, Januari 19, 2026, yaliyofungwa na Mohamed Damaro, Duke Abuya, Prince Dube, Pacome Zouzoua, Mudathir Yahya na Laurindo Dilson Maria ‘Depu’.
Kwa maana hiyo, Yanga inakutana na Mashujaa ikiwa na kumbukumbu nzuri pia, huku kwa upande wa kikosi hicho cha maafande kikikabiliwa na mwenendo usioridhisha, baada ya kucheza mechi nne mfulu-lizo za Ligi Kuu Bara hadi sasa bila ya ushindi.
Katika mechi hizo nne ilizocheza Mashujaa FC bila ya kushinda, imepoteza mbili na kutoka pia sare mbi-li, huku mara ya mwisho kwa kikosi hicho kushinda ilikuwa ni ushindi wa bao 1-0, dhidi ya TRA United ikicheza nyumbani, Mei 4, 2026.
Mbali na hilo, ila Mashujaa inakabiliwa na rekodi mbovu, kwani timu hiyo ya maafande tangu ipande Ligi Kuu Bara msimu wa 2023-2024, haijawahi kuifunga Yanga kwani zimekutana mara tano na kuchap-wa zote, ikiruhusu mabao 17 na kufunga matatu.
Katika mechi 25 za msimu huu wa 2025-2026, Yanga imeshinda 18, sare sita na kupoteza moja ikiongoza msimamo na pointi 60, huku kwa upande wa Mashujaa FC ikiwa nafasi ya 11 na pointi 27, baada ya kushinda tano, sare 12 na kupoteza nane.
MBEYA CITY v MTIBWA SUGAR
Mechi nyingine ya mapema saa 8:00 mchana itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, itazikutanisha Mbeya City dhidi ya kikosi cha Mtibwa Sugar, huku timu hizo zote zikiwa hazina mwenendo wa kuridhisha kwa siku za hivi karibuni.Mbeya City inayoshika nafasi ya 14 na pointi 22, imecheza mechi 25 hadi sasa na kati ya hizo imeshinda tano, sare saba na kupoteza 13, huku Mtibwa Sugar ikiwa ya 12 na pointi zake 27, baada ya kushinda sita, sare tisa na kupoteza 10.
Timu hizo zinakutana zikiwa na mwenendo usioridhisha na Mbeya City imecheza mechi nne mfululizo za Ligi Kuu bila ya ushindi, tangu mara ya mwisho kwa kikosi hicho kilipoifunga maafande wa Tanzania Prisons kwa mabao 2-1, Mei 4, 2026.
Kwa upande wa Mtibwa Sugar imecheza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu bila ya ushindi na imepoteza moja na kutoka sare pia moja, huku mara ya mwisho kwa timu hiyo kushinda ni ushindi mabao 4-3, dhidi ya KMC FC, Mei 14, 2026.
Mechi ya mzunguko wa kwanza zilipokutana, Mtibwa Sugar ilishinda kwa mabao 2-1, Januari 21, 2026, yaliyofungwa na George Chota dakika ya 21 na Said Mkopi dakika ya 63, huku la Mbeya City likifungwa na nyota, Eliud Ambokile dakika ya 45+2.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa Mbeya City, Salum Mayanga alisema licha ya timu hiyo ku-ruhusu idadi kubwa ya mabao hadi sasa, ila kwa muda aliokaa na wachezaji mazoezini amesahihisha makosa hayo na kuboresha safu yote ya ushambuliaji.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mkenya Yusuf Chippo alisema sababu ya mwenendo mbaya wa timu hiyo ni kutokana na baadhi ya wachezaji kukumbwa na majeraha kwa mechi zilizopita, ingawa kwa sasa wamerejea wote na wapo tayari kucheza.
JKT TZ v SINGIDA BS
Mechi ya mwisho kwa leo itapigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni saa 12:30 jio-ni na JKT Tanzania iliyo nafasi ya tano na pointi 38, itapambana na Singida Black Stars inayoshika nafasi ya nne na pointi 41.
JKT haijashinda mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara baada ya kutoka zote sare, huku mara ya mwisho kushinda ilikuwa ni ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Mbeya City, Mei 9, 2026, kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Kwa upande wa Singida Black Stars inaingia na morali kubwa zaidi baada ya mechi ya mwisho kuifunga Mbeya City mabao 4-1, kwenye Uwanja wa Airtel, Singida, Mei 26, 2026, japo raundi ya kwanza JKT Tanzania ilishinda bao 1-0, Januari 20, 2026.
Katika mechi hiyo ya raundi ya kwanza kati ya timu hizo iliyopigwa Januari 20, 2026, Singida ikiwa uwan-ja wa nyumbani, ilishindwa kutamba na kuchapwa bao 1-0, lililofungwa na kiungo mshambuliaji nyota wa JKT, Salehe Karabaka dakika ya 81.
JIUNGE NA SOGA COMMUNITY
MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI
What's Your Reaction?
Like
0
Dislike
0
Love
0
Funny
0
Wow
0
Sad
0
Angry
0
Comments (0)