Dar Leopards kukiwasha tamasha la raga

Jun 10, 2026 - 22:15
0 0
Dar Leopards kukiwasha tamasha la raga

By  Victoria Melkiad

Mwananchi Communications Limited

IKIWA zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa Tamasha la Touch Rugby Tournament, waandaaji wa mashindano hayo, Dar Leopards RFC wamewaomba mashabiki wa michezo huo kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Ufundi, Mikocheni ulioko Jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuzikutanisha timu 20 kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki yatafanyika Jumamosi, Juni 13 kuanzia asubuhi hadi jioni, huku ushindani mkubwa ukitarajiwa kutoka kwa timu zinazowania kumng'oa bingwa mtetezi Karen Crusaders.

Mbali na ubingwa wa jumla, waandaaji wametangaza zawadi maalumu zitakazoongeza hamasa kwa washiriki. Kutakuwa na tuzo za mchezaji bora wa kiume, mchezaji bora wa kike, mchezaji bora wa vijana pamoja na mkongwe bora wa mashindano hayo.

Katika kuongeza upekee wa tukio hilo, washindi watatunukiwa medali za kipekee zilizotengenezwa kwa ubunifu wa sanaa ya Tingatinga, hatua inayolenga kuonyesha utambulisho wa Kitanzania sambamba na kuenzi mchango wa sanaa katika michezo.

Mmoja wa viongozi wa Dar Leopards, Victoria Beach ameeleza kuwa kila kitu kipo tayari kwa ajili ya siku hiyo huku ukisisitiza kuwa tamasha hilo si kwa wachezaji pekee bali pia kwa familia na wadau wa michezo wanaotaka kupata burudani ya mwisho wa wiki.

Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0