September 3, 2026

DAR ES SALAAM: MSANII muigizaji maarufu wa Tanzania, Vincent Kigosi ‘Ray’ na mzazi mwenzake, mwigizaji Chuchu Hans, wamejaliwa kupata mtoto wao wa pili, ambaye ni mtoto wa kike aliyepewa jina la Cute Elsie.

Ray amemtambulisha rasmi mtoto huyo kwa jina hilo, akisema majukumu ya kuwa baba wa mtoto wa kike tayari yameanza.

Ameeleza namna jina hilo lilivyopatikana, Ray amesema lilizua mjadala ndani ya familia, huku mtoto wao wa kwanza wa kiume, Jaden, akiwa tayari amependekeza jina Elsie.

Kwa mujibu wa Ray, baada ya mjadala huo familia iliamua kutumia njia ya kura kwa kuandika majina kwenye vikaratasi na kisha kuyachagua. Hatimaye, Jaden alishinda kura hiyo, hivyo familia ikaamua mtoto huyo aitwe Cute Elsie.

Ray pia alitumia fursa hiyo kufanya mzaha kuhusu jina hilo, akifafanua kuwa halina uhusiano wowote na “Hers President” wa Yanga, akitania kwa namna yake.

Kwa upande wake, Chuchu Hans amemshukuru Mungu pamoja na watu wote waliomtakia heri na kumuombea kupata mtoto wa kike.

Amesema maombi hayo yamejibiwa na Mungu, ambaye amemjalia mtoto huyo na kumletea “rafiki na dada” mpya, huku akiamini kuwa ndugu yake Hudaa angefurahia pia ujio wa mtoto huyo.

Chuchu pia amewashukuru The Edra’s kwa kumrahisishia maandalizi ya ujio wa mtoto, akisema alipata mahitaji mbalimbali aliyohitaji kwa ajili ya mwanaye.

Ujio wa Cute Elsie unaifanya familia ya Ray na Chuchu kuwa na watoto wawili, Jaden akiwa mtoto wao wa kwanza na sasa wameongezewa mtoto wa kike.

Hongera Ray Kigosi na Chuchu Hans kwa kupata mtoto wa kike, Cute Elsie. Mungu amjalie afya njema, maisha marefu na baraka tele.

The post Jina la Cute Elsie lashinda first appeared on SpotiLEO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *