Ronaldo Kuongoza Kizazi cha Wachezaji Wakongwe Marekani 2026
Global Publishers June 5, 2026 0 Comments
SHARE THIS:
![]()
Wachezaji saba wenye umri wa miaka 40 na zaidi wanatarajiwa kushiriki kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026, jambo linaloonyesha uimara na maisha marefu ya soka kwa baadhi ya nyota wakubwa duniani.
Miongoni mwa wachezaji hao ni Cristiano Ronaldo ambaye akiwa na miaka 41 anatarajiwa kuweka historia kwa kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya sita.
Golikipa wa Scotland, Craig Gordon, ndiye atakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kwenye mashindano hayo akiwa na miaka 43.
Wengine wanaotarajiwa kushiriki ni Luka Modriฤ wa Croatia, Manuel Neuer wa Ujerumani, Edin Dลพeko wa Bosnia na Herzegovina pamoja na Guillermo Ochoa wa Mexico ambaye pia anatarajiwa kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya sita.
Aidha, golikipa Vozinha wa Cape Verde naye anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi hicho katika ushiriki wa kwanza wa taifa hilo kwenye Kombe la Dunia.
SHARE THIS:
JIUNGE NA SOGA COMMUNITY
MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI โ NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.
โ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
โ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
โ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
โ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI
What's Your Reaction?
Like
0
Dislike
0
Love
0
Funny
0
Wow
0
Sad
0
Angry
0
Comments (0)