Taifa Stars yapata pigo Morocco

Jun 04, 2026 - 13:15
0 0
Taifa Stars yapata pigo Morocco

ByΒ  Mwandishi Wetu

Mwananchi Communications Limited

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepata pigo baada ya kufutwa kwa ratiba ya michezo yake ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Uganda na Rwanda kutokana na uwepo wa tishio la ugonjwa wa Ebola.

Mamlaka za uongozi nchini Morocco ilipokuwa kuchezwe mechi hizo mbili za Stars imetangaza kuzuia kuzuia kwa michezo yote ya kimataifa iliyokuwa ifanyike nchini humo kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) ilisema Uganda imefuta mechi zake hizo kutokana na tahadhari ya masuala la Afya.

ZENG 01

UgandaΒ  maarufu kwa jina la 'The Cranes', ilikuwa na mechi mbili za kirafiki dhidi ya Tanzania na Madagascar, ambazo zilikuwa zichezwe jijini Marrakech, nchini Morocco wiki hii.

Hata hivyo, wakati Uganda ikitangaza uamuzi huo, tayari Tanzania na Madagascar, zilikuwa zimeshawasili jijini Marrakech, tayari kwa mechi hizo mbili.

ZENG 03

Uamuzi huo, utaifanya Tanzania kusalia na mchezo mmoja pekee wa kirafiki dhidi ya Rwanda, utakaopigwa Juni 9, baada ya ule wa Juni 5 dhidi ya Uganda kufutwa.

Taarifa zaidi zinasema, uamuzi huo wa Uganda unakuja wakati ambao taifa hilo likikumbwa na kesi za uwepo wa maradhi ya Ebola, ikiripotiwa watu 15 wamekumbwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

Wakala aliyekuwa anasimamia uandaaji wa mchezo huo, amekutana na wakati mgumu juu ya uhakika wa afya kwa wachezaji wa timu hiyo dhidi ya maafisa wa Morocco.

Comments (0)

User
πŸ”’
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI β€” NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

βœ… HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
βœ… MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
βœ… KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
βœ… KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
βœ… KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0