Wabunge waliosafiri Morocco bila kibali, Zungu awapa siku nne wajieleze

Jun 04, 2026 - 11:15
0 0
Wabunge waliosafiri Morocco bila kibali, Zungu awapa siku nne wajieleze

Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Zungu ametoa siku nne kwa wabunge waliokwenda Morocco bila kibali cha Spika wajieleze huku akitoa onyo kwa wabunge watoro bungeni.

Wabunge hao ni sehemu ya mashabiki waliokwenda Morocco kushuhudia fainali ya Mataifa Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Senegal.

Mechi hiyo ilichezwa katika Uwanja Uwanja wa Prince Moulay Hassan, Rabat na vijana wa Senegal kuibuka na ushindi wa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Spika Zungu ametoa agizo hilo leo Alhamisi, Juni 4, 2026, bungeni jijini Dodoma akimtaka Katibu wa Bunge kuwaandikia barua mara moja na wajibu vinginevyo hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Mbali na waliokwenda Morocco, Spika Zungu amesema kumekuwa na utoro ndani ya Bunge ambao hauwezi kuvumiliwa wakiwemo wengine kusalimiana.

"Lakini mawaziri nao wanaondoka wote, najua wana vibali vyao lakini Waziri Mkuu, hawa wasipewe vibali vya ziara wote, akitoka waziri basi naibu awepo Bungeni siyo wanakosekana wote," amesema Zangu.

Kingine amebainisha kuna baadhi ya wabunge wanaomba vibali wakisema wanakwenda majimboni lakini wanakwenda nje ya nchi.

Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0