August 27, 2026

MONACO: Timu 36 zinazoshiriki UEFA Champions League 2026/27 Leo Agosto 27, 2026 zitafahamu wapinzani wao wanane watakapatikana kupitia droo itakayofanyika usiku wa leo huko Monaco.

Timu hizo zimegawanywa katika Pots nne, kila moja ikiwa na timu tisa. Mfumo huo unalenga kuhakikisha kila klabu inapata wapinzani wawili kutoka kila Pot.

Kila timu itacheza jumla ya mechi nane dhidi ya wapinzani nane tofauti, ikiwa na michezo minne nyumbani na minne ugenini.

Miongoni mwa vigogo waliopo Pot 1 ni Arsenal, Manchester City, Liverpool, Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, PSG, Inter Milan na Atlético Madrid, hivyo kuna uwezekano wa kuona mechi kubwa mapema.

Manchester United ipo Pot 2 pamoja na Borussia Dortmund, Roma, Sporting CP, Aston Villa, Porto, Club Brugge, Real Betis na PSV Eindhoven.

Pot 3 na Pot 4 nazo zina timu zenye ushindani, ikiwemo Napoli, Galatasaray, Villarreal, Feyenoord, Lille, Stuttgart, Como, Lens na Slavia Prague.

Baada ya mechi nane, timu nane bora kwenye msimamo zitafuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora, huku zinazomaliza nafasi ya 9 hadi 24 zikicheza play-off.

Kwa hiyo, macho ya mashabiki wa soka duniani sasa yako kwenye droo hiyo, wakisubiri kuona ni vigogo gani watakutana katika hatua ya ligi ya Champions League msimu huu.

The post Watakaokutana UEFA Champion League 2026/27 kujulikana leo first appeared on SpotiLEO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *