BTS kuitikisa Los Angeles
LOS ANGELES: Jiji la Los Angeles limetan… Read the rest
The post BTS kuitikisa Los Angeles first appeared on SpotiLEO.
LOS ANGELES: Jiji la Los Angeles limetangaza kuanzia Septemba 1 hadi 8 ni wiki ya Kundi maarufu la muziki kutoka Korea Kusini linalojulikana kwa jina la BTS, hatua inayolenga kutambua mchango wa kundi hilo katika muziki na utamaduni wa kimataifa, hiyo ni baada kundi hilo kutonekana jukwaani kwa miaka takribani mitano
Kwa mujibu wa taarifa kutoka jiji hilo, BTS imepewa heshima hiyo kutokana na mchango wake katika kueneza muziki wa Korea Kusini na utamaduni wa Asia katika sehemu mbalimbali duniani.

Pia, ujumbe wa kundi hilo unaohusisha upendo, matumaini na kujikubali umeendelea kuwafikia mamilioni ya mashabiki kutoka mataifa mbalimbali.
Ujio wa BTS umeifanya Los Angeles kujaa mashabiki wanaofahamika kama ARMY, ambao wamejitokeza kwa wingi kushuhudia kundi hilo likirejea kwenye jukwaa la jiji hilo.
Maonesho hayo yamekuwa miongoni mwa matukio makubwa ya burudani katika jiji hilo, huku mashabiki wakionesha shauku kubwa kupitia mitandao ya kijamii na shughuli mbalimbali zinazohusishwa na BTS.
Ziara hiyo imekuwa na umuhimu wa kipekee kwa mashabiki wa Los Angeles, kwani inatajwa kuwa moja ya kurejea kwa BTS kwenye jukwaa hilo baada ya takribani miaka mitano tangu kundi hilo lilipotumbuiza katika ukumbi wa SoFi mwaka 2021.
Kurejea kwa BTS kama kundi kamili kumeongeza hamasa miongoni mwa mashabiki duniani, huku ARIRANG World Tour ikiendelea kuwa moja ya matukio yanayofuatiliwa kwa karibu katika ulimwengu wa muziki mwaka huu.
Baada ya Los Angeles, BTS inatarajiwa kuendelea na ratiba yake ya ziara katika miji mbalimbali duniani, ikiwa ni sehemu ya kurejea kwake kwenye shughuli za pamoja kama kundi kamili.
The post BTS kuitikisa Los Angeles first appeared on SpotiLEO.
