Filamu ya marehemu Onwenu kutoka Ijumaa
LAGOS: Filamu ya kihistoria ya Nollywood,… Read the rest
The post Filamu ya marehemu Onwenu kutoka Ijumaa first appeared on SpotiLEO.
LAGOS: Filamu ya kihistoria ya Nollywood, “Properties of the Gods,” ambayo inatajwa kuwa miongoni mwa kazi za mwisho za marehemu mwanamuziki na mwigizaji Onyeka Onwenu, inatarajiwa kuanza kuoneshwa katika kumbi za sinema nchini Nigeria Ijumaa, Septemba 4, 2026.
Filamu hiyo, iliyotayarishwa na Joseph Okechukwu, imepewa umuhimu wa pekee kutokana na ushiriki wa Onwenu katika moja ya nafasi zake za mwisho kwenye filamu kabla ya kifo chake.
Mtayarishaji wa filamu hiyo, Joseph Okechukwu, ametangaza kuwa Septemba 4 itatambuliwa kama ‘Onyeka Onwenu Day’, huku shughuli mbalimbali zikipangwa kwa ajili ya kuenzi mchango wa nyota huyo katika tasnia ya burudani nchini Nigeria.

Kabla ya kuanza kuoneshwa kwa filamu hiyo, usiku maalum wa kumbukumbu na heshima kwa Onyeka Onwenu umepangwa kufanyika Septemba 3.
Pia, badala ya kufanya uzinduzi mkubwa wa kawaida wa filamu, Okechukwu aliamua kusitisha hafla hiyo kutokana na vifo vya baadhi ya waigizaji waliokuwa sehemu ya mradi huo.
Okechukwu amesema fedha ambazo zingetumika katika premiere zitatumika katika shughuli za kuwafariji na kuwaheshimu familia za waigizaji waliofariki, akiwemo Onyeka Onwenu na Cynthia Okereke.
Mtayarishaji huyo amesema kufanya sherehe kubwa wakati familia za waigizaji hao zikiwa bado katika kipindi cha maombolezo hakungekuwa jambo sahihi.
“Properties of the Gods” ni filamu ya kihistoria inayogusia suala la mfumo wa Osu katika jamii ya Igbo, pamoja na athari zake katika maisha, mahusiano na jamii.
Filamu hiyo inalenga kuibua mjadala kuhusu mila, ubaguzi, utambulisho na namna baadhi ya desturi za zamani zinavyoendelea kuathiri jamii.
The post Filamu ya marehemu Onwenu kutoka Ijumaa first appeared on SpotiLEO.
