Tamasha la Filamu la Venice laanza
ITALIA: TAMASHA la 83 la Filamu la Venice… Read the rest
The post Tamasha la Filamu la Venice laanza first appeared on SpotiLEO.
ITALIA: TAMASHA la 83 la Filamu la Venice limeanza rasmi leo Septemba 2, 2026, nchini Italia, likiwakutanisha mastaa wakubwa wa filamu kutoka maeneo mbalimbali duniani katika moja ya matamasha makubwa na yenye ushawishi katika tasnia ya sinema.
Miongoni mwa matukio yaliyovuta zaidi macho ya mashabiki ni kutunukiwa kwa mwigizaji na mtengenezaji wa filamu, George Clooney, tuzo ya Golden Lion for Lifetime Achievement kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu.
Tamasha hilo limeanza huku likiwa na mkusanyiko wa filamu zinazogusa masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa, yakiwemo vita, mabadiliko ya tabianchi, uhamiaji pamoja na migogoro ya kimataifa.
Miongoni mwa filamu zinazoshindana kuwania tuzo ya juu ya Golden Lion ni Ink, iliyoongozwa na Danny Boyle na kuigiza na Guy Pearce pamoja na Jack O’Connell. Filamu hiyo inasimulia kisa kinachohusiana na Rupert Murdoch na ununuzi wa gazeti la The Sun mwaka 1969.
Mbali na Clooney, mastaa wengine wanaotarajiwa kuonekana katika tamasha hilo ni pamoja na Robert Pattinson na mwigizaji mkongwe Ellen Burstyn, ambaye pia anatarajiwa kuheshimiwa kwa tuzo ya Golden Lion.
Tamasha la Venice la mwaka huu linatarajiwa kuendelea hadi Septemba 12, huku wadau wa filamu wakilitazama kama sehemu muhimu ya kuibua filamu zinazoweza kuingia katika kinyang’anyiro cha tuzo kubwa za kimataifa, ikiwemo Oscars.
The post Tamasha la Filamu la Venice laanza first appeared on SpotiLEO.
