Keffe D akutwa na hatia mauaji ya Tupac
NEVADA: MAHAKAMA imemkuta Duane ‘Ke… Read the rest
The post Keffe D akutwa na hatia mauaji ya Tupac first appeared on SpotiLEO.
NEVADA: MAHAKAMA imemkuta Duane ‘Keffe D’ Davis na hatia ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa nyota wa Hip Hop, Tupac Shakur, yaliyotokea miaka 30 iliyopita huko Las Vegas.
Katika hoja za kuhitimisha kesi, upande wa mashtaka ulieleza Keffe alikuwa kiongozi mkuu wa South Side Compton Crips, genge lililomuwinda Tupac na kusimamia tukio hilo.
Walieleza ingawa Keffe, 63 hakufyatua risasi zilizomuua Pac, lakini alipanga shambulio hilo lililotajwa la kulipiza kisasi na kutoa silaha iliyotumiwa na mpwa wake, Orlando ‘Baby Lane’ Anderson, kumpiga risasi rapa huyo.
Imeelezwa, mauaji hayo yalifuatia baada ya ugomvi uliotokea saa chache kabla ambapo Pac na wenzake walipigana na Anderson katika casino moja mjini Las Vegas.
Sehemu muhimu ya ushahidi wa upande wa mashtaka ilitokana na Keffe kuzungumzia nafasi yake katika tukio hilo wakati wa mahojiano ya siri na polisi mwaka 2008.
Baadaye alitoa maelezo zaidi kupitia makala, mahojiano, podcast na kitabu chake cha mwaka 2019, Compton Street Legend.
Aidha, kupitia dokumentari ya Sean Combs: The Reckoning ya mwaka jana, Keffe anaonekana kuzungumzia mauaji hayo namna yalivyopangwa na kiasi cha pesa alichoahidiwa.
Upande wa utetezi ulisema maelezo ya Keffe ya tukio hilo katika kitabu chake yalikuwa ‘hadithi ya kubuni’, akiongeza chumvi katika simulizi ili kujipatia umaarufu na kuuza vitabu, na kwamba hakuna rekodi za uchunguzi wa ushahidi wa moja kwa moja wa Keffe kuhusika.
Hata hivyo, majaji walimkuta Keffe na hatia ndani ya saa chache baada ya kuanza kujadili ushahidi wa kesi hiyo na atahukumiwa Oktoba 13, mwaka huu ingawa ana mpango wa kukata rufaa.
Pac au Makaveli alipigwa risasi Septemba 7, 1996, akiwa ndani ya gari na pamoja na Bosi wa Lebo ya Death Row Records, Marion “Suge” Knight na kufariki baada ya siku sita akiwa na umri wa miaka 25.
The post Keffe D akutwa na hatia mauaji ya Tupac first appeared on SpotiLEO.
