Mabula: Ukurasa mpya, lengo lilelile
ALGIERS: MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Tan… Read the rest
The post Mabula: Ukurasa mpya, lengo lilelile first appeared on SpotiLEO.
ALGIERS: MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania, Alphonce Mabula, ameanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka nchini Algeria baada ya kutambulishwa rasmi na klabu ya JS Kabylie.
Mabula, aliyesajiliwa na JS Kabylie akitokea Samaxi FK ya Azerbaijan, amesema yupo tayari kuanza safari hiyo mpya huku akiwa na mtazamo uleule wa kufanya vizuri na kuendelea kupambana ndani ya uwanja.
Kupitia ujumbe wake baada ya kutambulishwa, Mabula amewashukuru mashabiki wa JS Kabylie kwa mapokezi ya upendo waliyompa, akisema tayari anajisikia kuwa nyumbani.
“Ukurasa mpya, lakini lengo ni lilelile. Nawashukuru mashabiki wa JS Kabylie kwa mapokezi yenu mazuri. Tayari najisikia niko nyumbani na siwezi kusubiri kuanza kazi,” amesema Mabula.
Mabula anakuwa sehemu ya JS Kabylie akitarajiwa kutumia uzoefu wake kuongeza nguvu katika kikosi hicho na kuendelea kujenga jina lake katika soka la kimataifa.
The post Mabula: Ukurasa mpya, lengo lilelile first appeared on SpotiLEO.
