Shime: Tumerejesha nguvu kuivaa Brazil
WARSAW: KOCHA wa timu ya Taifa ya Wanawak… Read the rest
The post Shime: Tumerejesha nguvu kuivaa Brazil first appeared on SpotiLEO.
WARSAW: KOCHA wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, Bakari Shime, amesema kikosi chake kimepata muda wa kurejesha nguvu na kuzoea hali ya hewa ya Poland baada ya kuwasili nchini humo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia la Wanawake U20 mwaka 2026.
Akizungumzia maandalizi ya kikosi nchini Poland, Shime amesema mazoezi waliyofanya yalilenga kuwaondolea wachezaji uchovu, kuwazoesha hali ya hewa ya eneo hilo pamoja na kukumbushana baadhi ya mbinu watakazotumia katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Brazil.

Amesema hali ya hewa si mbaya kama walivyotarajia awali na wamepata muda wa kuizoea.
“Hali ya wachezaji kwa ujumla ni nzuri, tunatarajia kutumia siku zilizobaki kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo huo, kujiweka tayari kwa kila kitu,”amesema.
Ameongeza kuwa wataendelea kuwasaidia wachezaji kurejesha nguvu kwa kutumia njia mbalimbali ili kuingia uwanjani wakiwa katika hali nzuri.
Mchezo huo wa ufunguzi unatarajiwa kuchezwa Jumamosi kwenye dimba la Bielsko Biala, nchini Poland.
The post Shime: Tumerejesha nguvu kuivaa Brazil first appeared on SpotiLEO.
