Priscilla: Maisha yangu yalipata maana nilipokutana na Jux
DAR ES SALAAM: MKE wa msanii wa Bongo Fle… Read the rest
The post Priscilla: Maisha yangu yalipata maana nilipokutana na Jux first appeared on SpotiLEO.
DAR ES SALAAM: MKE wa msanii wa Bongo Fleva, Juma Mkambala ‘Jux’, Priscilla Ojo Mkambala, ameeleza namna uwepo wa mume wake ulivyobadili maisha yake, akisema maisha yalipata maana siku aliyokutana na msanii huyo.
Priscilla ametoa kauli hiyo kupitia ujumbe maalum amemwandikia Jux katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, akieleza kuwa kumpenda mume wake ni jambo rahisi zaidi ambalo amewahi kulifanya katika maisha yake.
Katika ujumbe huo, Priscilla amemshukuru Jux kwa namna anavyompenda na kumthamini, huku akisema tangu awali aliamini kuwa mume wake angekuwa baba bora.
Hata hivyo, amesema kumshuhudia Jux akiwa baba wa mtoto wao, Rakeem, kumemzidi matarajio yote aliyowahi kuwa nayo.
Priscilla amesema namna Jux anavyompenda na kumjali mtoto wao imemfanya ampende zaidi mume wake, lakini safari hii kwa namna tofauti na mpya.
“Nilijua ungekuwa baba mzuri, lakini kukuona ukiwa baba kwa Rakeem kumepita kila kitu nilichowahi kufikiria,” ni sehemu ya ujumbe wake.
Aidha, Priscilla amesema anajivunia kuwa mke wa Jux, hasa kwa namna anavyomshuhudia akikua na kuwa mwanaume wa kipekee, huku akiendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kupitia kazi zake.
Ujumbe huo wa Priscilla umeonyesha upande wa familia wa Jux, huku akitumia siku yake ya kuzaliwa kumueleza hadharani namna anavyothamini upendo wao na nafasi yake kama mume na baba wa mtoto wao.
The post Priscilla: Maisha yangu yalipata maana nilipokutana na Jux first appeared on SpotiLEO.
