Sepetu ajiweka mbali na watu batili
DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Movies, We… Read the rest
The post Sepetu ajiweka mbali na watu batili first appeared on SpotiLEO.
DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Movies, Wema Sepetu, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kutoa ujumbe unaoashiria kuchoshwa na watu wasiokuwa wa kweli katika maisha yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sepete ameweka ujumbe katika Instagram Story ameandika: “No more Fake People Please”, akionekana kuomba kuwa karibu na watu wanaokuwa wa kweli na waaminifu kwake.
Ujumbe huo umeibua hisia na maswali mbalimbali miongoni mwa mashabiki wake, huku baadhi wakijiuliza iwapo kuna jambo limetokea katika mahusiano yake ya kirafiki au amekutana na hali iliyomfanya kufikisha ujumbe huo hadharani.
Hata hivyo, Wema hakufafanua zaidi kuhusu ujumbe huo wala kutaja mtu au watu ambao alikuwa akiwaelekezea kauli yake.
Kauli hiyo imeendelea kuzua maneno kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki wakisubiri kuona kama mwigizaji huyo atatoa ufafanuzi zaidi kuhusu kile alichomaanisha.
The post Sepetu ajiweka mbali na watu batili first appeared on SpotiLEO.
