Beki Simba amfuata Msuva Iraq

Jul 10, 2026 - 03:15
0 0
Beki Simba amfuata Msuva Iraq

Klabu ya Al Talaba anayocheza Mtanzania, Simon Msuva, imetangaza kuingia mkataba wa miaka miwili na beki aliyemaliza muda wake ndani ya Simba, Chamou Karaboue.

Al Talaba imempa beki huyo raia wa Ivory Coast mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine.

Msimu uliomalizika wa 2025-2026, wakati wa usajili wa dirisha dogo la Januari 2026, Simba ilimtoa Chamou kwa mkopo kwenda TRA United, aliyomaliza nayo msimu huku mkataba wake na Simba wa miaka miwili ukimalizika Juni 2026.

Chamou msimu ujao atakuwa kikosi kimoja na Msuva anayeitumikia klabu hiyo huu ukienda mwaka wa tatu.

Chamou alikuwa mmoja wa mabeki muhimu wakati Simba inafundishwa na Kocha Fadlu Davids msimu wa 2024-2025 ambapo timu hiyo ilipofika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Baada ya Fadlu kuondoka mwanzoni mwa msimu wa 2025-2026, taratibu Chamou akaanza kupoteza nafasi.

Kocha Steve Barker baada ya kutua Simba Desemba 2025, aliamua kumuondoa Chamou kupitia dirisha dogo la usajili, kisha nafasi yake akasajiliwa Ismael Toure ambaye aliingia moja kwa moja kwenye kikosi cha Simba, akionyesha ubora mkubwa kwenye ukuta wa Wekundu hao wa Msimbazi.

Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0