Ligi Kuu Bara 2026/27 Kuanza Agosti 16, Usajili Waanza Rasmi

Jul 08, 2026 - 19:15
0 0
Ligi Kuu Bara 2026/27 Kuanza Agosti 16, Usajili Waanza Rasmi

Global Publishers July 8, 2026 0 views 0 Comments

SHARE THIS:

Mashabiki wa soka nchini wanatarajia kushuhudia msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/2027 ukianza rasmi Agosti 16, 2026, huku ukitarajiwa kumalizika kabla ya Juni 1, 2027.

Ratiba hiyo imepangwa mapema ili kutoa nafasi ya maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), ambazo zitafanyika kwa pamoja nchini Tanzania, Kenya na Uganda kuanzia Juni 19 hadi Julai 18, 2027.

Kutokana na mashindano hayo makubwa ya bara Afrika, waandaaji wa ligi wameamua kuhitimisha msimu mapema ili kuruhusu maandalizi ya timu za taifa pamoja na shughuli nyingine zinazohusiana na AFCON.

Aidha, mashabiki wanatarajiwa kupata ratiba ya michuano ya Ngao ya Jamii kabla ya kutolewa kwa ratiba kamili ya Ligi Kuu ya msimu wa 2026/2027.

Wakati huo huo, dirisha kubwa la usajili kwa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara limefunguliwa rasmi Julai 6, 2026, na litafungwa Agosti 15, 2026 saa 5:59 usiku.

Kipindi hiki kinazipa klabu nafasi ya kuimarisha vikosi vyao kwa kusajili wachezaji wapya kabla ya msimu mpya kuanza.

Kwa kuanza kwa dirisha la usajili, mashabiki sasa wanaendelea kufuatilia kwa karibu harakati za timu zao katika kusajili nyota wapya zitakazoongeza ushindani wa msimu wa 2026/2027.

SHARE THIS:

Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0