Justin Bieber, Shakira, Madonna na BTS Kutumbuiza Fainali ya Kombe la Dunia 2026

NEW YORK – Nyota wa muziki duniani Justin Bieber ataungana na Shakira, Madonna na kundi la BTS kutumbuiza kwenye onyesho maalum la mapumziko ya kipindi cha kwanza (halftime show) katika fainali ya Kombe la Dunia 2026, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza.
Onyesho hilo la dakika 11 litafanyika wakati wa fainali ya Kombe la Dunia itakayochezwa Julai 19 karibu na Jiji la New York, Marekani. Litakuwa likisimamiwa na mwanamuziki Chris Martin wa bendi ya Coldplay na limeandaliwa kwa mtindo unaofanana na maonesho maarufu ya Super Bowl Halftime Show.
Mbali na Bieber, wasanii wengine watakaotumbuiza ni nyota wa Afrobeats Burna Boy, kondakta wa muziki kutoka Venezuela Gustavo Dudamel, pamoja na PS22 Chorus, kwaya ya wanafunzi wa shule ya msingi kutoka Staten Island, New York, ambao wataungana na Coldplay jukwaani.
Onyesho hilo litakuwa sehemu ya kampeni ya FIFA Global Citizen Education Fund, inayolenga kukusanya dola milioni 100 kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa elimu na kuendeleza mchezo wa soka kwa watoto duniani.
“Kombe la Dunia lina uwezo wa kuunganisha dunia kwa namna ambayo hakuna tukio lingine linaweza kufanya. Ninafurahi kuwa sehemu ya onyesho hili, na zaidi kufahamu kuwa linasaidia watoto wengi kupata elimu,” alisema Justin Bieber kupitia taarifa rasmi.
Ushiriki wa Burna Boy umepewa uzito wa kipekee kutokana na kuwa mmoja wa waimbaji wa wimbo rasmi wa Kombe la Dunia 2026, “Dai Dai”, aliouimba kwa kushirikiana na Shakira. Wimbo huo umeunganisha ladha ya Afrobeats na midundo ya Kilatini, huku ukitaja baadhi ya mataifa na mastaa wakubwa wa soka wanaoshiriki mashindano hayo.
“Kombe la Dunia ni moja ya matukio machache yanayoiunganisha dunia nzima. Kuiwakilisha Afrika katika halftime show ya kwanza kabisa ya fainali ya Kombe la Dunia ni heshima kubwa na jukumu ninalolichukua kwa uzito,” alisema Burna Boy.
Mbali na wasanii hao, onyesho hilo litawashirikisha pia wahusika maarufu wa Sesame Street, akiwemo Kermit the Frog na Miss Piggy, wakitarajiwa kuongeza burudani kwa mashabiki watakaofuatilia fainali hiyo duniani kote.
Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kwa FIFA kuandaa onyesho rasmi la halftime show wakati wa fainali, hatua inayolenga kuleta burudani ya kiwango cha kimataifa sambamba na mchezo wenyewe.
SHARE THIS:
JIUNGE NA SOGA COMMUNITY
MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI
What's Your Reaction?
Like
0
Dislike
0
Love
0
Funny
0
Wow
0
Sad
0
Angry
0
Comments (0)