Kaze amtema straika Yanga Sauzi

Jul 10, 2026 - 03:15
0 0
Kaze amtema straika Yanga Sauzi

By  Khatimu Naheka

Reporter

Mwananchi Communications Limited

Klabu ya Sekhukhune ya Afrika Kusini, imetangaza kuwatema wachezaji wake watatu akiwemo straika mmoja wa zamani wa Yanga.

Sekhukhune ambayo sasa inafundishwa na kocha Cedric Kaze ikimchukua baada ya kuachana na Kaizer Chiefs, katika wachezaji watatu iliowatema yumo Andy Boyeli.

Boyeli msimu uliopita aliitumikia Yanga nusu msimu kwa mkopo akitokea Sekhukhune, kabla ya kurudishwa dirisha la Januari 2026 kutokana na mabingwa hao wa Tanzania kushindwa kukubaliana na kiwango chake.

Leo Julai 9, 2026, Sekhukhune imemtema Boyeli ikimpa 'Thank you' baada ya kudumu klabuni hapo kwa misimu miwili.

Mbali na Boyeli ambaye mpaka anaondoka Yanga aliifungia mabao mawili pekee, pia Sekhukhune imewatema Tresor Tshibwabwa huku Shaune Mogaila akiondoka kwa makubaliano maalum ya kuachana kwa pande mbili.

Kaze ameanza hesabu za kusuka kikosi kipya akitaka kutafutiwa wachezaji wenye ubora zaidi kuziba nafasi walizokuwa wakizitumikia watatu hao.

Kocha huyo raia wa Burundi, amepewa mkataba mgumu akitakiwa kuibakiza timu hiyo kwenye nafasi  kumi za mwanzo kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Msimu wa 2025-2026, timu hiyo ilimaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 44 baada ya kucheza mechi 30.

Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0