Ufaransa Yaiondoa Morocco, Yatinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia

Jul 10, 2026 - 12:15
0 0
Ufaransa Yaiondoa Morocco, Yatinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia

Ndoto ya Morocco ya kurudia mafanikio ya kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia imefikia tamati baada ya kufungwa mabao 2-0 na Ufaransa katika mchezo wa robo fainali uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Morocco ilionyesha uimara mkubwa, huku kipa Yassine Bounou akiokoa mkwaju wa penalti wa Kylian Mbappe katika dakika ya 25 na kufanya save nyingine kadhaa muhimu zilizoiweka timu yake kwenye mchezo kwa muda mrefu.

Hata hivyo, shinikizo la Ufaransa hatimaye lilizaa matunda kipindi cha pili. Mbappe aliifungia Les Bleus bao la kwanza dakika ya 60 kwa shuti la kifundi lililomshinda Bounou, kabla ya Ousmane Dembele kuongeza la pili dakika ya 66 kwa shuti kali lililotoka nje ya eneo la penalti.

Morocco ilijaribu kujibu kupitia mashambulizi ya haraka, lakini ilikosa mshambuliaji wa asili kufuatia majeraha ya Ismael Saibari, hali iliyopunguza makali yao mbele ya lango.

Kocha Mohamed Ouahbi alifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Sofyan Amrabat, Soufiane Rahimi, Zakaria El-Ouahdi, Gessime Yassine na Amine Sbai, lakini juhudi hizo hazikuweza kubadili matokeo.

Ushindi huo unaifanya Ufaransa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya tatu mfululizo, huku Morocco ikiaga mashindano baada ya kuandika historia nyingine kwa kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kufika robo fainali ya Kombe la Dunia mara mbili mfululizo (2022 na 2026).

Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0