Aziz Ki: Kazi ngumu hulipa
DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Yanga, Aziz Ki, … Read the rest
The post Aziz Ki: Kazi ngumu hulipa first appeared on SpotiLEO.
DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Yanga, Aziz Ki, amesema kazi kwa bidii, nidhamu na kujitolea ni msingi wa mafanikio, akieleza kufurahishwa na ushindi walioupata pamoja na timu yake.
Aziz Ki ametoa kauli hiyo kupitia ujumbe akiwapongeza wachezaji wenzake kwa ushindi katika mchezo wa jana dhidi ya Fountain Gate wa mabao 2-0 huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kupambana katika michezo inayofuata.
Nyota huyo alicheza mchezo wake wa kwanza jana tangu kurejea kunako klabu hiyo na kutoa pasi ya bao alililofunga Peter Shalulile. Bao lingine lilifungwa na Mudathir Yahya.
“Kazi ngumu, nidhamu na kujitolea daima hulipa mwishoni. Najivunia timu hii na ushindi huu. Tuendelee kusonga mbele,” amesema Aziz Ki.
Nyota huyo pia ameacha ujumbe wenye kuonesha uhusiano wake na mashabiki wa Yanga akisema: “Mwananchi one day, Mwananchi forever akimaanisha mwananchi siku moja, mwananchi milele.”
Aziz Ki ameonesha kuwa uhusiano wake na Yanga ni wa kudumu, akisisitiza kuwa hata baada ya siku moja kuwa Mwananchi, ataendelea kuwa Mwananchi milele.
The post Aziz Ki: Kazi ngumu hulipa first appeared on SpotiLEO.
