Barker: Sasa ni zamu ya Ligi ya Mabingwa
DAR ES SALAAM: BAADA ya kuiongoza Simba k… Read the rest
The post Barker: Sasa ni zamu ya Ligi ya Mabingwa first appeared on SpotiLEO.
DAR ES SALAAM: BAADA ya kuiongoza Simba kupata ushindi wa tano mfululizo kwenye Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu Steven Barker amesema sasa anahamisha nguvu zake kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, akisisitiza kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya licha ya kuanza vizuri msimu.
Kauli ya Barker inakuja baada ya timu yake kuifunga Geita Gold mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu jana kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuhyo.
Barker amesema amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na kikosi chake katika ushindi huo, akieleza kuwa walidhibiti mchezo, walitengeneza nafasi za kutosha na kutumia vizuri nafasi walizopata.
“Ushindi wa michezo mitano mfululizo ni jambo zuri kwetu na ni matokeo mazuri, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Ni mwanzo mzuri wa msimu. Sasa ni wakati wa kuelekeza mawazo kwenye Ligi ya Mabingwa na kwa muda tuweke pembeni ligi hadi tutakaporejea kucheza baada ya wiki kadhaa,” amesema.
Kocha huyo amesema ushindi wa michezo mitano mfululizo ni mwanzo mzuri kwao, lakini amesisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa mbele yao, hivyo wanapaswa kuendelea kuboresha kikosi.
The post Barker: Sasa ni zamu ya Ligi ya Mabingwa first appeared on SpotiLEO.
