Tems: Mimi siimbi Afrobeats
LAGOS: Mwanamuziki mashuhuri, Tems ameele… Read the rest
The post Tems: Mimi siimbi Afrobeats first appeared on SpotiLEO.
LAGOS: Mwanamuziki mashuhuri, Tems ameeleza wazi kuwa licha ya yeye kutoka Afrika haimaanishi kuwa anaimba muziki wa Afrobeats.
Tems, 31 ameeleza hayo alipokuwa akihojiwa katika Kipindi cha Hot97 na kufafanua kuwa anaimba aina mbili za muziki; R&B na Alternative Afro-Soul.
Ameeleza huwa anashangazwa na kila msanii wa Afrika kutambulishwa na blogs na nchi za Magharibi kama msanii wa Afrobeats wakati kila mmoja anaimba muziki wake.
“Mimi si msanii wa Afrobeats. Nachokiona kila msanii anayetoka Afrika anatambulishwa na mitandao na nchi nyingine kuwa anaimba Afrobeats.
“Mimi nikifanya muziki huwa siwazi kuhusu ‘genre’ ya huo muziki na mwisho nikimaliza kutoa wimbo unakuta ni wa R&B lakini unatajwa kama Afrobeat,” alisema Tems.
Tems anayewania Tuzo za MTV VMA 2026, amesisitiza kuwa Afrika ni kama sehemu nyingine duniani, inafanya miziki ya aina mingi ingawa Afrobeats ni utambulisho wao.
Mwisho.
The post Tems: Mimi siimbi Afrobeats first appeared on SpotiLEO.
