Caf yaanza ukaguzi wa miundombinu kuelekea Afcon 2027
DAR ES SALAAM: WAJUMBE kutoka Shirikisho … Read the rest
The post Caf yaanza ukaguzi wa miundombinu kuelekea Afcon 2027 first appeared on SpotiLEO.
DAR ES SALAAM: WAJUMBE kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wanaounda kamati mbalimbali za maandalizi ya mashindano, wameanza ziara ya siku tatu ya kukagua miundombinu na huduma zitakazotumika katika mashindano ya AFCON 2027 yanayotarajiwa kufanyika Tanzania, Kenya na Uganda.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo jana Dar es Salaam, wataalamu hao wamefanya kikao na Kamati ya Maandalizi ya Mashindano (LOC), ambapo wamejadili maandalizi na maeneo mbalimbali yanayohitaji kupewa kipaumbele kuelekea mashindano hayo.

Baada ya kikao, wajumbe hao wameendelea na ukaguzi wa miundombinu ikiwemo viwanja vya michezo, huku sekta ya afya ikiangaziwa kuwa miongoni mwa maeneo muhimu katika maandalizi ya AFCON 2027.
Katika eneo hilo, wataalamu wa CAF wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kujionea huduma na taasisi zake mbalimbali, ikiwemo Taasisi ya Mifupa (MOI) pamoja na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), kwa lengo la kutathmini uwezo wa huduma za afya katika kuhudumia mahitaji ya mashindano.
Ziara hiyo inahusisha wataalamu kutoka kamati mbalimbali za CAF, zikiwemo zinazohusika na miundombinu ya viwanja, afya na huduma za matibabu, usafiri na usafirishaji, malazi, usalama pamoja na maeneo mengine muhimu katika uendeshaji wa mashindano.
Wajumbe hao wanatarajiwa kuendelea na ziara Zanzibar kesho, Septemba 2, 2026, ambapo watafanya ukaguzi wa miundombinu na huduma mbalimbali zinazohusiana na maandalizi ya mashindano hayo.
The post Caf yaanza ukaguzi wa miundombinu kuelekea Afcon 2027 first appeared on SpotiLEO.
