Photos from AzamSports's post

Jun 05, 2026 - 17:15
0 0
Photos from AzamSports's post
MILIONI 400 ZATENGWA KWA AJILI YA IMBEJU– NDONDO CUP: Mdhamini mkuu wa msimu wa 13 wa Imbeju – Ndondo Cup 2026, taasisi ya CRDB Bank Foundation, amesema wametenga zaidi ya shilingi milioni 400 zitakazotumika kuendesha ligi hiyo inayowahusisha vijana kutoka mtaani zikiwamo zaidi ya shilingi milioni 100 zitakazotolewa kama zawadi kwa timu, wachezaji na mashabiki.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa ligi hiyo inayotekelezwa mpaka ngazi ya mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa amesema msimu huu unaleta fursa juu ya fursa kwa kila mdau wa Imbeju – Ndondo Cup.

“Mashindano ya Imbeju - Ndondo Cup 2026 yataanzia mashinani hadi ngazi ya mkoa. CRDB Bank Foundation imewekeza jumla ya shilingi milioni 400 ambazo zinajumuisha gharama za uendeshaji pamoja na zawadi. Bingwa wa mashindano haya atapata shilingi milioni 30 na mshindi wa pili atapata shilingi milioni 15 na kwenye kila hatua timu inayofuzu itapewa kiasi cha fedha.

Pia, kutakuwa na zawadi kwa mchezaji bora, mfungaji bora, beki bora na kipa bora wa Imbeju Ndondo Cup 2026 pamoja na shabiki ua kikundi maahiri kwa kushangilia,” amesema Tully.

Tully amesema katika kila mechi, mchezaji bora wa mechi (man of the match) atapata shilingi 100,000 na shabiki mahiri pia atapata shilingi 100,000. Fedha hizi zitawekwa kwenye Akaunti ya Imbeju ya kila muhusika hivyo kutoa fursa juu ya fursa hali inayotimiza kaulimbiu ya Imbeju – Ndondo cup 2026 isemayo ‘Jiongeze.’

Na msimu wa michuano utakapokamilika, mchezaji bora atajinyakulia shilingi milioni 3 huku golikipa na beki bora wakipata shilingi milioni 1 kila mmoja. Zawadi hizi zote, Tully amesema zinakusudia kufungua fursa kwa timu na wachezaji kutoka mtaani kuianza vyema safari yao ya kujijenga kiuchumi.

#NdondoCup2026









Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0