Uhamiaji FC yaachana na nyota saba!

Jul 10, 2026 - 17:15
0 0
Uhamiaji FC yaachana na nyota saba!

By  Zuleikha Fatawi

Reporter

Mwananchi Communications Limited

WAKATI timu zikijiandaa na msimu ujao wa 2026-2027 kwa kuboresha vikosi vyao, Uhamiaji imeamua kuachana na wachezaji saba.

Hayo yamebainishwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdul Saleh Mohamed wakati akizungumza na Mwanaspoti.

Kocha huyo amesema wachezaji hao wapo ambao hawakuonesha kiwango kizuri, huku wengine uwezo wao umepungua.

Pia, amesema wapo wachezaji ambao walisajiliwa msimu wa 2025-2026 kwa lengo la kuisaidia timu, lakini kwa bahati mbaya hawakufikia malengo.

“Timu ina mpango wa kuacha wachezaji kama saba kwasababu wamepungua viwango na wengine tulikuwa nao hawajatuonesha kile ambacho tulikitaka ndani ya uwanja,” amesema.

Mbali na hilo, kocha huyo, amesema katika kuboresha kikosi hicho watafanya usajili wa beki wa kati na mshambuliaji kwani hayo ndio maeneo ambayo hayapo vizuri.

Uhamiaji ni miongoni mwa timu zilizoanza vizuri msimu wa 2025-2026 kwa kushika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar, lakini ilimaliza msimu nafasi ya tano baada ya kusuasua ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 30, ikishinda 15, sare sita na kupoteza 10 huku ikifunga mabao 46 na kuruhusu 27.

Comments (0)

User
🔒
SALAMA NA RAHISI KUJIUNGA

JIUNGE NA SOGA COMMUNITY

MASHABIKI WA MICHEZO NA MATUKIO DUNIANI WANAKUTANA HAPA. HAKUNA FUJO, HAKUNA MATUSI — NI MAZUNGUMZO YA MAANA NA MARAFIKI WAPYA.

✅ HAKUNA MADHARA KUJIUNGA NA CHAT YETU
✅ MFUMO UNAZUIA CHATS ZISIZOFAA
✅ KUBLOCK USER ASIYE NA MAADILI
✅ KUMSHITAKI NA KUMFUKUZA MTUMIAJI MBAYA
✅ KUFOLLOW NA KUBEFRIEND WATUMIAJI WENYE MAADILI

What's Your Reaction?

Like Like 0
Dislike Dislike 0
Love Love 0
Funny Funny 0
Wow Wow 0
Sad Sad 0
Angry Angry 0